Kwa kweli najaribu kujizuia kumkosoa au kuangalia kwa ukaribu kauli za Waziri Mkuu Mpya Bw. Mizengo Pinda na kama nilivyosema awali kuwa bado yeye na timu yake nawapa muda angalau wa miezi sita hivi ili waweze kujionesha kuwa wanaweza kweli kukabili changamoto za Taifa letu tutawaweka kwenye kundi la "wale wale".
Walipotangazwa nilisema kuwa ninawapa asilimia 100 ya imani yangu kwao na mimi kama wengine tunasubiri ni kwa kiasi gani wataitunza hiyo imani siku kwa siku katika utendaji wao
Kwa vile siyo lengo langu kuonesha udhaifu wa kauli za Waziri Mkuu na maana iliyofichika ndani yake, ninajikuta basi leo katika kuwaza kuuliza tu kama kauli za Waziri Mkuu kwa vyombo vya habari zinapimwa vizuri au ni za papo kwa hapo?"
Kwamba ni kwa kiasi gani Waziri mkuu anapozungumzia suala la mapendekezo ya Bunge kuhusu suala la Richmond yeye anasema hivi: Kama Spika ataona ni vema kunipa nafasi katika Bunge hili, nitatoa taarifa ya baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa kwa hatua za awali, na kama nitakosa nafasi, Bunge lijalo taarifa yote ya mapendekezo inaweza ikatolewa ikiwa imekamilika
Mwanzoni nilidhani kuwa yeye kama Waziri Mkuu na ambaye ndiye msimamizi wa shughuli za serikali Bungeni ana uwezo wa kumtaarifu Spika kuwa ana taarifa muhimu kuhusu Richmond. Iweje sasa amemrudishia mpira spika? Ina maana kama Spika asipompa nafasi ndiyo imetoka hiyo?
Na kuhusu suala la EPA alisema kitu kimoja ambacho nadhani kinahitaji majibu kuhusu imani ya Waziri Mkuu kuhusu Mahakama zetu au maana nzima ya kuamua kufuata mahakama ili kupata au kutafuta haki. Alisema kwanini waliamua kutaka fedha zirudishwe kwanza "Usipojipanga vizuri unaweza kukurupuka kuwashtaki na wakakushinda, hivyo utapoteza vyote, kesi umeshindwa na fedha hujapata, sasa serikali kwanza inaona cha muhimu ni kupata fedha zake, mambo mengine baadae"
Sasa mimi nauliza, kama hana la kusema ni lazima aseme kitu ilimradi aseme? Kama jambo hajalipangia kauli nzuri kwanini kutumia kauli zenye utata kama hizi? Je, ameanza kupinda maneno? Au tuendelee kumpa muda kidogo ajifunze kutokana na makosa. Je anaye mwandishi wa hotuba?

HABARI HII IMETUMWA NA MWANAKIJIJI

No comments:
Post a Comment