Thursday 24 April 2008

MUM katika Bonanza



Picha ya juu wanafunzi wa chuo kikuu cha Waislamu Morogoro wakishangilia ushindi wa dada zao walioibuka washindi katika mchezo wa netball dhidi ya chuo cha MOTCO.

Picha ya pili mshambuliaji hatari wa timu ya soka ya MUM Haroub Said akitafakari kabla ya timu yake kupambana na timu ya chuo kikuu cha Mzumbe.

Picha ya tatu wachezaji wa timu ya netball ya MUM wakipeana mawaidha wakati wa mpambano wao dhidi ya MOTCO. Michuano hiyo ya Bonanza kwa vyuo vya elimu ya juu mkoa wa Morogoro inafanyika katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Tumejiandaa na ongezeko la bei ya chakula?

Ndugu zangu, kuna uwezekano mkubwa kwamba itakapofika kiangazi mwaka huu, Taifa letu linaweza kujikuta kwenye upungufu mkubwa wa chakula ambao siyo tu unatishia maisha ya watu wetu bali pia unashusha hadhi na utu wa mwanadamu. Hakuna kitu kinachomdhalilisha mwanadamu na kuweza kumfanya awe mtu kama njaa.

Ni njaa ndiyo inayoweza kumfanya mtu aukane urithi wake wa kwanza kama alivyofanya Esau na ni njaa ambayo ilikuwa inatumika tangu enzi za kale kama silaha ya mwisho ya vita ambayo inalazimisha watu kusalimu amri. Tanzania tutakabiliwa na njaa ambayo chanzo chake si ukame.
Mara nyingi (kama siyo zote) njaa husababishwa na ukame na vita. Hata hivyo njaa ambayo naweza kuiangalia toka mbali na inayosogelea kama simba anyatiaye haitokani na mambo hayo bali makubwa mawili.
a. Kupanda kwa bei ya chakula duniani.
Habari za leo ni kuwa bei ya chakula duniani imepanda kwa haraka kuliko wakati wowote ule na hivyo kusababisha ugumu wa kupatikana kwa chakula.
Yaliyotokea Haiti na Misri siku chache zilizopita ni dalili ya ubaya wa hali hiyo. Kwa wale walioko Dar au maeneo yenye masoko ya kudumu na kwenye mialo mbalimbali kanda ya ziwa wanaweza kutusaidia kutuambia kama kumeanza kutokea mabadiliko yanayoonekana ya bei ya chakula siku hizi chache zilizopita
b. Mvua za Masika
Hata hivyo, naamini kwa upande wa Tanzania kitakachosababisha njaa sana ni hii mvua ambayo imeharibu mashamba na mazao ya watu kiasi kwamba baadhi ya maeneo ambayo kwa kawaida yana chakula cha kutosha yanaweza kujikuta yanahamia mwaka huu. Kama mpunga wa Kyela utakuwa umeathirika kama Dr. Mwakyembe alivyosema kwenye mahojiano yake nami kuna uwezekano kuwa Mwaka huu bei ya Mchele nayo itapanda na hivyo kufanya nafaka hiyo ianze kuwa adimu na kupatikana kwa wachache.

Maeneo ambayo mchele ndiyo chakula kikuu na pia zao la biashara watajikuta wanakabiliwa na upungufu wa fedha za kununulia hata vitu vingine na hivyo kusubiri chakula cha misaada. Kwa vile tunajua haya yote na ziada; tufanye nini ili tujiandae na njaa ijayo?
Habari hii ni kwa mujibu wa Mwanakijiji anayepatikana katika mtanadao wa
http://mwanakijiji.podOmatic.com

Monday 21 April 2008

MUM yaichapa Ardhi katika Bonanza


Picha ya kwanza wachezaji wa MUM FC wakipata mawaidha kutoka kwa kocha wao Malyo Njedengwa Cheto aliyevaa fulana nyeupe na track ya bluu wakati wa mapumziko.Picha ya pili baadhi ya viongozi na mashabiki wa MUM wakiwapa mawili matatu wachezaji wao muda mfupi kabla ya kuanza ngwe ya mwisho ya mpambano wao dhidi ya Ardhi.


Leo timu ya soka ya Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM FC) imeanza vyema mashindano ya Bonanza la vyuo vya mkoa wa Morogoro yanayojulikana kama CRDB-MOHLISO Bonanza yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri. Katika mchezo huo MUM iliibuka na ushindi wa magoli 2-1. wafungaji wa mabao ya MUM ni Haroub Said na Seif Hamza.

Kujiuzulu kwa Chenge usiwe mwisho!


Ni kweli yawezekana kuwa kujiuzulu Uwaziri kumepokelewa kwa furaha na wengi (mimi mmoja wao). Yawezekana kwa kufanya hivyo uchunguzi utakuwa huru (sidhani alikuwa anazuia uchunguzi anyway); yawezekana kujiuzulu kwake kumekuwa ni kitulizo cha kelele dhidi ya ufisadi; Yawezekana kujiuzulu kwake kumeonesha ufisadi wa viongozi wa serikali ya JK na hivyo kumuondoa kumeonesha jitihada za kusafisha serikali hiyo;


Hata hivyo, hadi hivi sasa CCM haijalipa gharama yoyote ya viongozi wake kuhusishwa na ufisadi na hakuna wakati hadi hivi sasa ambao wao kama CCM wamechukua hatua za viongozi wa serikali waliofanya vitendo vya ufisadi wakiwa ni wanachama wake. Ni kwa sababu hiyo basi naamini kujiuzulu kwa Chenge toka serikalini hakutoshi bali lazima kufuatiwe na kujiuzulu toka Ubunge. Kwanini?a. Kiasi cha fedha anachodaiwa kukutwa nacho kingeweza kuleta mabadiliko makubwa kwa watu wa Jimbo lake lakini aliwaficha wapiga kura wake.b. Kwa kukiita kiasi hicho "vijisenti" kwa kisingizio cha "usukuma wake" ni tusi kwa wasukuma wengine ambao hawajui maana ya "vijisenti" hasa baada ya yeye mwenyewe kuelezea kuwa "kila mtu ana kiwango chake".


c. Mwakilishi wa wananchi anapotajwa na kuhusishwa na kitendo cha matumizi mabaya ya nafasi yake, nafasi ambayo imetokana na kuchaguliwa na wananchi hao, basi anapojiuzulu nafasi yake basi hana budi kuachia kiti chake ili ampishe mtu mwingine kushika nafasi hiyo. Bw. Chenge amewaangusha wapiga kura wake, na amekiletea aibu kubwa chama chake. Kati ya wote walioatajwa katika tuhuma za ufisadi ni yeye pekee ambaye tunajua angalau kiasi gani che fedha kimefichwa huko Jersey. Kwa sababu hiyo basi Chenge siyo tu ajiuzulu Uwaziri kama alivyofanya bali pia ajiuzulu Ubunge wake na Uwakilishi wake ili mwana CCM au mtu mwingine aweze kuwawakilisha wananchi wa Bariadi Magharibi.JIUZULU UBUNGE BW. CHENGE, UMEKUWA AIBU YA TAIFA LETU!


Habari hii ni kwa mujibu wa Mwanakijiji anayepatiakana katika mtandao wa http://mwanakijiji.podomatic.com/

Sunday 20 April 2008

Prof. Hamza Njozi

Makamu Mkuu wa Chuo cha Waislamu Morogoro (MUM) Prof. Hamza Njozi akizungumza na waandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Abood mjini Morogoro

Hii ndiyo adha ya ongezeko la bei ya Mafuta




Mwenge wa Olympic Tanzania


Hapa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein akipokea Mwenge wa Olympic ulipowasili nchini Tanzania hivi karibuni.

Chenge mbona anatuchengua!


Chenge ni bilionea wa kutupwa ambaye kwake shilingi Bilioni moja anayodaiwa kuificha huko Marekani ni sawa na "vijisenti" vichache. Hivi tatizo letu liko wapi? Je yawezekena kuwa chenge ni dalili tu ya tatizo? Je eye ni kiongozi pekee wa TAnzania ambaye amewekeza mabilioni ya shilingi kwenye akaunti za kigeni? Je ajiuzulu au na yeye anaweza akalia kuwa amefanywa "Bangusilo" wa rada!?
Hata hivyo, habari zilizopatiakana hivi punde zinaeleza kuwa tayari mheshimiwa Chenge amejiuzulu wadhifa wa Waziri wa Miundombinu.


Habari hii ni kwa mujibu wa Mwanakijiji anayepatikana katika mtandao wa http://mwanakijiji.podomatic.com/