Friday 11 April 2008

Mambo ya KP leo


Pinda ameanza kupinda maneno?

Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda

Kwa kweli najaribu kujizuia kumkosoa au kuangalia kwa ukaribu kauli za Waziri Mkuu Mpya Bw. Mizengo Pinda na kama nilivyosema awali kuwa bado yeye na timu yake nawapa muda angalau wa miezi sita hivi ili waweze kujionesha kuwa wanaweza kweli kukabili changamoto za Taifa letu tutawaweka kwenye kundi la "wale wale".
Walipotangazwa nilisema kuwa ninawapa asilimia 100 ya imani yangu kwao na mimi kama wengine tunasubiri ni kwa kiasi gani wataitunza hiyo imani siku kwa siku katika utendaji wao
Kwa vile siyo lengo langu kuonesha udhaifu wa kauli za Waziri Mkuu na maana iliyofichika ndani yake, ninajikuta basi leo katika kuwaza kuuliza tu kama kauli za Waziri Mkuu kwa vyombo vya habari zinapimwa vizuri au ni za papo kwa hapo?"
Kwamba ni kwa kiasi gani Waziri mkuu anapozungumzia suala la mapendekezo ya Bunge kuhusu suala la Richmond yeye anasema hivi: Kama Spika ataona ni vema kunipa nafasi katika Bunge hili, nitatoa taarifa ya baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa kwa hatua za awali, na kama nitakosa nafasi, Bunge lijalo taarifa yote ya mapendekezo inaweza ikatolewa ikiwa imekamilika
Mwanzoni nilidhani kuwa yeye kama Waziri Mkuu na ambaye ndiye msimamizi wa shughuli za serikali Bungeni ana uwezo wa kumtaarifu Spika kuwa ana taarifa muhimu kuhusu Richmond. Iweje sasa amemrudishia mpira spika? Ina maana kama Spika asipompa nafasi ndiyo imetoka hiyo?
Na kuhusu suala la EPA alisema kitu kimoja ambacho nadhani kinahitaji majibu kuhusu imani ya Waziri Mkuu kuhusu Mahakama zetu au maana nzima ya kuamua kufuata mahakama ili kupata au kutafuta haki. Alisema kwanini waliamua kutaka fedha zirudishwe kwanza "Usipojipanga vizuri unaweza kukurupuka kuwashtaki na wakakushinda, hivyo utapoteza vyote, kesi umeshindwa na fedha hujapata, sasa serikali kwanza inaona cha muhimu ni kupata fedha zake, mambo mengine baadae"
Sasa mimi nauliza, kama hana la kusema ni lazima aseme kitu ilimradi aseme? Kama jambo hajalipangia kauli nzuri kwanini kutumia kauli zenye utata kama hizi? Je, ameanza kupinda maneno? Au tuendelee kumpa muda kidogo ajifunze kutokana na makosa. Je anaye mwandishi wa hotuba?


HABARI HII IMETUMWA NA MWANAKIJIJI

Mtoto wa Ajabu



Chinga wa India

Machinga wa India wakipambana na askari.

'Breaking News'

Habari ambazo zinaingia mida hii kutoka Dar zinasema kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta baada ya kukutana leo imeamua kuwatimua wakurugenzi wake watatu kwa kile kinachoaminika ni kuvujisha siri za shirika hilo hususan zihusiano na vitendo vya kifisadi.
Habari za ufisadi kwenye shirika hilo zilitemwa kwenye mtandao huu wa JF siku chache zilizopita. Hata hivyo kwa wale "wanaojua" habari hizi hazikutoka kwa afisa yeyote wa juu ndani ya shirika hilo isipokuwa baadhi ya Watanzania ambao wamechoshwa na hujuma na vitendo vya kifisadi.
Kama ufukuzwaji huo utathibitishwa hii itakuwa ni mara nyingine ambapo JF imetumiwa kisingizio cha kufukuza watu ili kutishia watumishi wa umma wasifichue uovu kwenye taasisi za umma na ambazo ni nyeti. Miezi michache iliyopita shirika la ndege la ATC nalo lilitimua watumishi wake watano kwa kisingio cha kuvujisha siri za ununuzi wa dege la Airbus na vitendo vya kifisadi ndani ya shirika hilo.
Wakati huo huo mojawapo ya Vyuo Vikuu vya Tanzania nacho kimemfuta kazi mmoja wa wahadhiri wake waandamizi kwa kile amacho viongozi wa chuo hicho wanadai kuwa ni "pressure" toka juu hasa baaada ya mhadhiri huyo mwishoni mwaka jana kujitokeza hadharani na kumnyoshea kidole cha ufisadi mmojawapo wa mawaziri na kumtaka ajiuzulu.
Kama tabia hii ya "kufukuza fukuza" itaendelea bila kukomeshwa mara moja, Taifa la Tanzania litakuwa limeanzisha utawala wa vitisho na utamaduni wa kuziba habari za vitendo vya kifisadi kwa kutishia retaliation kwa mtu yeyote yule.
Hadi hivi sasa haijajulikana ni kwa kiasi gani sheria ya "Whistleblowing" imefikia na ni lini sheria hiyo itaanza kuwalinda Watanzania ambao wanaibua vitendo vya kifisadi, kuhujumu uchumi, rushwa, na ukiukwaji wa maadili katika sehemu zao za kazi.
Title: KLH News Episode: Bila CCM Madhubuti? - Mwalimu alisema kweli...

HABARI HII IMETUMWA NA MWANAKIJIJI
anayepatikana katika mtandao wa http://mwanakijiji.podOmatic.com

Wednesday 9 April 2008

Mahojiano

Hapa waandishi wa habari wa Jarida la Panorama la nchini Marekani wakifanya mahojiano na aliyekuwa Waziri wa Maji Dk. Shukuru Kawambwa ambaye sasa ni Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Tekonojia ya Habari.

Athari za Mvua Moro

Hili ni tope lililosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Hapa ni katika manispaa ya mji wa Morogoro.

Kipigo cha Liverpool dhidi ya Arsenal





Picha zote zinaonesha jinsi timu ya Liverpool ilivyoigaragaza Arsenal jumla ya magoli 4-2 katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya hapo jana nchini Uingereza.

Naomi


Mwanamitindo Naomi akiwa katika mwendo wa 'mapozi'

Kila mtu kivyake


Kibuyu chirizi

Watoto wakinawa uso kwa kutumia maji yanayotoka katika Kibuyu Chirizi. Shule za Msingi zimeshauriwa kuwa na utaratibu utakaowawezesha wanafunzi kunawa maji usoni mara kwa mara kwa lengo la kuepuka ugonjwa wa Trachoma nchini Tanzania.

Hapa hakuna jinsi tena


Hapa ni kitabu tu!


Tuesday 8 April 2008

UDOM

Hiki ndicho Chuo Kikuu kipya cha Serikali Dodoma (UDOM) kilichopo mkoani Dodoma.

Kuku

Muuza kuku akiwaonesha wateja kuku anayemuuza. Hapa ni Kibaigwa mkoani Dodoma.

Monday 7 April 2008

Kumbukumbu

Tanzania na Rwanda leo ziko katika maadhimisho ya kukumbuka ya vifo vya viongozi wao. Wakati watanzania hususan Wazanzibar wanakumbuka kuuawa kwa Rais wao wa kwanza Abeid Amani Karume Wanyarwanda wao wanakumbuka kifo cha aliyekuwa Rais wao Juvenal Habyarimana aliyeuawa pamoja na yule wa Burundi Cyprian Ntayamira katika shambulio la ndege karibu kabisa na mji wa Rwanda Kigali . Viongozi hao wawili walikuwa wakitoka katika mkutano wa usuluhishi wa mgogoro katika nchi zao nchini Tanzania.

Tunawatakia kila la kheri

Ndani ya Kariakoo 'Bongo'


Maji ya Mvua yanavunwa hivi!


Utamaduni wa Mtanzania

Hapa kikundi cha ngoma kikifanya vitu vyake katika maonesho ya Wiki ya Maji yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

Zanzibar Airport

Hapa nipo na waandishi wenzangu katika uwanja wa ndege wa Zanzibar mwaka 2000, wa kwanza kulia Meck Mdaku, mimi, Nicolas Mbaga(TVT) na Emanuel Herman(Mtanzania).

Sunday 6 April 2008

Haya ni mambo ya 'kawa'


Hapo vipi tena!


Mambo ya Mwenge wa Olympic London leo


Leo katika jiji la London palikuwa hapatoshi wakati Mwenge wa Olympic ulipokuwa ukikimbizwa katika maeneo tofauti ya jiji hilo.