Monday 14 April 2008

Mvua za 'Bongo' si mchezo




Rostam, Richmond na siri ya watu wawili!


Sakata la Richmond na mtikisiko wake bado havijaisha Bungeni. Kuna kila dalili kuwa yaliyotokea Bungeni mwezi wa pili na kusababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu na kuvunjika kwa baraza la Mawaziri hayakuwa mwisho. Kuna kila dalili kuwa kuna baadhi ya watu ambao waliumizwa na hadi hivi sasa hawajakubali "yaishe"

Miongoni mwa watu ambao kwa hakika waliumizwa hisia zao, hadhi na sifa zao ni Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz (CCM) ambaye wakati wa matukio hayo alidai kuwa ripoti iliyosomwa na Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge Mhe. Harrison Mwakyembe (Kyela - CCM) haikuwa sahihi na akadai kama vile wengine kuwa hakutendewa haki.

Juhudi za kujisafisha kwa wahusika mbalimbali wa Richmond zimekuwa zikiendelea na kwa namna fulani jukumu kubwa zaidi linamuangukia Bw. Rostam ambaye aidha kwa kujitwisha mwenyewe au kukubali kutumika inaonekana amekuwa akitumia kila aina ya njia upande mmoja kujibu mashambulizi ya wapinzani kwa kutumia vyombo vyake vya habari na upande wa pili kutilia shaka utendaji mzima wa Kamati Teule na hivyo kujaribu kuhoji maamuzi yote yaliyotolewa Bungeni

Katika kikao kinachoendelea cha Bunge alitakiwa aje kutoa maelezo yake na kujibu hoja za Wabunge na kutoa utetezi wake. Mwishoni mwa juma alikuwa amejiandaa kutoa utetezi huo lakini kwa kile kinachodaiwa kuwa ni "unyeti" wa utetezi wake basi imeonekana si vyema kwa Bw. Rostam kujitetea Bungeni kwani italeta msukosuko mwingine nchini.

Kama hilo ni kweli au ni mojawapo ya karata za CCM binafsi siamini kuwa Rostam anaweza kusema chochote kile ambacho kinaweza kutuyumbisha kama Taifa na ambacho hatuwezi kukihimili. Tumeweza "kuchafuka kwa hali ya kisiasa Zanzibar", tumeweza kuhimila msiba wa Sokoine, tumeweza kuhimili "mizengwe" ya Kizota na kifo cha Katibu Mkuu Kolimba na kwa hakika tumeweza kuhimila kujiuzulu kwa WAziri Mkuu.

Naamini nchi yetu inaweza kuhimili msuko suko wowote ule wa kisiasa hata kama ni kujiuzulu kwa Rais aliyeko madarakani! Hata ikibidi Bunge zima kujiuzulu au kuvunjwa na kuitisha uchaguzi mwingine, TAifa letu lina uwezo wa kuhimili mambo hayo kwani Taifa ni kubwa zaidi kuliko kikundi fulani cha wanasiasa.

Wito wangu leo ni kuwa kama Rostam analo la kusema na aliseme sasa asinyamazishwe tena wala kupigwa mkwara na chama chake. Kamas anaona hakutendewa haki yeye kama Raia basi anayo haki ya kujisafisha hadharani badala ya kulazimika kukaa kimya. Asije akafikiri kuwa ana mpango wa kuzungumza "huko mbeleni" lakini ikatokea kuwa yeye na utetezi wake wakanyamaza "milele" kama alivyonyamaza Bi. Amina Chifupa ambaye naye alitaka kupewa nafasi ya kujitetea lakini akazibwa mdomo. Natoa wito; kama Rostam unaamini una hoja SIMAMA JITETEE NA JIELEZE.

Lakini swali kubwa ni Rostam ana nini ambacho kinampa nguvu ya kutia mwashawasha Bungeni? Je anatikisha kiberiti kuona kama kimejaa.

Habari hii ni kwa mujibu wa Mwanakijiji anayepatikana katika mtandao wa http://mwanakijiji.podomatic.com/

'Madent' wakipata Muhogo

Hapa wanafunzi wa Muslim University of Morogoro wakipata chakula cha muhogo jioni chuoni hapo.

Duuh! Mvua nayo balaa



Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro wakipita kwa taabu kukwepa madimbwi ya maji kuelekea darasani kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Mambo ya Samani za ndani


Wanawake nao!

Hii ilikuwa wakati wanawake walipofanya maandamano ya kupinga ziara ya Rais wa Marekani nchini Tanzania George Bush.

Sunday 13 April 2008

Man vs Arsenal na Liverpool vs Blackburn Rovers



Picha zote zinaonesha mechi baina ya Manchester United na Arsenal ambapo Man United imeibuka washindi kwa magoli 2-1 wakati Liverpool nayo imeichapa Blackburn Rovers mabao 3-1.

Wamasai katika Marathon


Pichani wamasai wakiwa katika Marathon nchini Uingereza.

Mafuriko Kyela

Pichani baadhi ya wananchi wakijaribu kuvuka mto. Kidaraja hicho sasa hakipitiki tena. Picha kwa hisani ya Mjengwa

Mvua za masika zimezidi kupamba moto nchini na zimekuwa zikisababisha mafuriko sehemu mbalimbali. Baadhi ya maeneo ambayo yamepata mafuriko ni pamoja na Vunjo, Same na Kyela. Hata hivyo hadi hivi sasa ni wilaya ya Kyela ambayo ina kata 15 ambazo kati ya hizo 11 zimepatwa na mafuriko makubwa .

Siku ya Jumamosi nimepata nafasi ya kuzungumza na Mbunge wa Jimbo la Kyela Dr. Harrison Mwakyembe (CCM) kuhusu athari za mafuriko hayo na mahitaji ya msaada. Kwa kifupi hali ilivyo ni kuwa:

a. Kaya 9000 hazina mahali pa kuishi, zimekosa chakula, au athari ya moja kwa moja iliyotokana na mafukio hayo

b. Hadi hivi sasa watu wawili wamefariki

c. Madhara makubwa katika mashamba ya mpunga kiasi kwamba kuna uwezekano kuwa kwa mara ya kwanza Kyela itahemea chakula mwaka huu.

d. Mvua kubwa namna hii hazijawahi kunyesha Kyela kwa karibu miaka thelathini sasa.

e. Juhudi za kuleta misaada zinaendelea ambapo JWTZ imepeleka kikosi chake cha Uhandisi, huku Msalaba Mwekundu wakiandaa misaada ya vitu mbalimbali.

Dr. Mwakyembe anaomba msaada wa Watanzania wote popote pale walipo kuweza kusaidia wananchi wenzao ambao ni kama wamepatwa na "Kimbunga cha Katrina" kwani wengi sasa wanaishi makanisani na kwenye mashule na afya zao ziko hatarini hasa kutokana na uwezekano mkubwa wa kuibuka mlipuko wa magonjwa yanayoambukizwa kwa maji kama typhoid, kuhara damu, salmonella, na pia ongezeko la Mbu wasababishao Malaria.

Kwa yeyote aliyeko Dar, unaweza kutuma mchango wako kupitia:
Kyela Development Fund MNB Bank House Acct No: 2013300198
Au Wasiliana na Dr. Mwakyembe kupitia simu Namba: 255 754 284130kwa maelekeo ya kuweza kutoa mchango wako kupitia yeye mwenyewe

Tafadhali sikiliza mahojiano yangu na Dr. Mwakyembe. KLH News imeahidi kutoa msaada wa Shilingi laki mbili kama sehemu ya jitihada za kuwasaidia wananchi wa Kyela.



Habari hii ni kwa mujibu wa Mwanakijiji anayepatikana katika mtandao wa
http://mwanakijiji.podomatic.com/