Friday 4 April 2008

Watanzania na Utalii Uk

Watanzania waishio Uingereza wamekuwa mstari wa mbele kutangaza utalii wa nchi yao kama wanavyoonekana pichani wakiwa na basi lenye matangazo.

CCM Ughaibuni

Hapa wana CCM wanaoishi nchini Uingereza wakiwa katika maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi.

Maafa ya Mererani

Wachimbaji wa Madini wa Mererani wakisubiri kuipokea miili ya watu waliokufa katika Mgodi wa madini wa Mererani mkoani Arusha.

Malima akipongezwa na Spika

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta (kushoto) Edward Lowassa (katikati) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adam Malima.

Haya mzee twende kazi!


Thursday 3 April 2008

Shaka Ssali

Mtangazaji maarufu wa Voice of America Shaka Ssali akipata kinywaji alipofanya ziara nchini Tanzania

Mambo gani tena haya!




Mambo ya ughaibuni




Punda afe mzigo ufike


Wednesday 2 April 2008

Hapa kazi tu!

Mpiga picha wa Kituo cha Televisheni Zanzibar (TVZ) Salehe Masoud akifanya kazi yake. Hapa ilikuwa katika mbuga ya Wanyama ya Mikumi mkoani Morogoro. Wa kwanza kushoto ni mwandishi wa habari maarufu kutoka Uingereza Vyonne Ridley na anayemfuatia ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM) Asiyatu Msuya.

Wasanii


Watoto hawa niliwakutana maeneo ya Mnazi Mmoja Dar es Salaam wakichora picha kwa ajili ya maonesho ya Wiki ya Maji.

Tufanyeje tena!

Hapa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark Mwandosya wakijadili jambo na Mkurugenzi wa DAWASA Bw. Mutalemwa. Hii ilikuwa katika mto Ruvu.

Duuuh! hapo vipi tena


Tuesday 1 April 2008

Prof. Mikidadi akiongea kwa hisia

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM) Prof. Jumanne Mikidadi mbunge mstaafu wa CCM akizungumza katika moja ya mihadhara yake.



Niko OK!


Prof Mwandosya akiwa Ruvu

Hapa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Mark Mwandosya akiwa katika ziara yake ya kutembelea Mtambo wa Ruvu. Hii ilikuwa ni siku yake ya kwanza kuanza kazi katika Wizara kufuatia kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa. Picha hii niliinasa nilipokuwa ziarani na mheshimiwa Waziri.


Utalii

Watalii wakiwa katika Mbuga ya wanyama Mikumi.

Ridley na Uislam

Bi. Vyonne Ridley akipata maelezo kuhusiana na maktaba ya Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM) kutoka kwa mkurugenzi wa maktaba ya chuo hicho Bw. Masawe (Kulia) huku Makamu Mkuu wa MUM Prof. Hamza Njozi akiangalia.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM) Prof. Hamza Njozi akimuongoza Bi. Ridley katika majengo ya idara ya Mawasiliano ya Umma ambapo huko kuna studio za Radio na Televisheni, Chumba cha Habari na chumba cha uhariri.




Bi. Vyonne Ridley




Waislamu nchini Tanzania wametakiwa kuungana pamoja ili kukabiliana na vitendo vyote vya ukandamizaji vinavyofanywa dhidi yao.

Hayo yalielezwa hivi karibuni na mwandishi maarufu kutoka Uingereza Bi. Vyonne Ridley wakati akihutubia maelfu ya waumini wa dini ya kiislamu katika mhadhara uliondaliwa na chuo kikuu cha waislamu Morogoro (MUM) uliofanyika ukumbi wa Star Light jijini Dar es Salaam.

Alisema, hivi sasa kumekuwepo ukandamizaji, uonevu na udhalilishaji unaofanywa dhidi ya nchi za kiislamu kutoka baadhi ya nchi hususan zile za magharibi jambo alilolieleza kuwa linahatarisha usalama wa waumini wa dini hiyo.

Bi. Ridley aliongeza kuwa, njia pekee ya kuweza kukabiliana na hali hiyo ni waislamu duniani kuwa na umoja kwa lengo la kuhakikisha hakuna ukandamizaji ama uonevu unaofanywa dhidi yao.



Mwandishi huyo wa habari maarufu kutoka Uingereza ambaye amesilimu Ukristo na kuwa Muislamu alisema, pamoja na awali kuelewa waislamu ni magaidi na watu hatari lakini alipotekwa na wanamgambo wa Taliban aligundua ni watu wakarimu tofauti na inavyoenezwa.

‘’Nilichogundua nilipotekwa na wanamgambo wa Taliban ni kuwa waislamu ni watu wakarimu, wazuri na wenye hekima tofauti na inavyooenezwa na baadhi ya nchi za magharibu kuwa ni watu hatari na magaidi’’ alisema Bi. Ridley.

Akiongea kwa hisia kali Bibi Ridley alibainisha kuwa, pamoja na kuelezwa waislamu ni magaidi lakini hadi hii leo mwandishi huyo hajapata tafsiri halisi ya neno gaidi kutoka kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair mbali na kuihitaji tafsiri hiyo mara kwa mara kutoka kwake.

Amewataka waumini wa dini ya kiiislamu kumtii mwenyezi mungu na kuyafuata mafundisho yake kwani anaamini kunusurika kwake alipotekwa huko Afighanistan ni uwezo wa mwenyezi Mungu na si mtu mwingine.


Katika mhadhara huo ukumbi wa Star Light ulifurika idadi kubwa ya watu huku baadhi yao wakimua kuondoka kutokana na kukosa nafasi. Hata pale Bibi Ridley alipomaliza kutoa mhadhara watu walitaka aendelee jambo lililomlazimu Makamu mkuu wa chuo cha waislamu Morogoro Prof. Hamza Njozi kuingilia kati na kuwasihi kuwa muda wa sala ulikuwa umefika na katika mambo yanayoweza kuahirisha sala mhadhara haukupewa nafasi.

Baada ya kauli hiyo ya Prof Njozi, wanawake walimfuata Bibi Ridley na kumzonga kwa shauku ya kutaka kusalimiana naye jambo lililomuweka katika wakati mgumu mgeni huyo ambaye hii ni mara yake ya kwanza kuitembelea Tanzania.

Baadhi ya waislamu waliozungumza na gazeti hili la Baraza wakati wa mhadhara huo waliomba Bi.Ridley kuendelea na ziara yake nchini na kuonana na makundi mbalimbali .

Bi. Ridley alikuja nchini kwa mwaliko wa Chuo kikuu cha waislamu Morogoro na kuanza ziara yake chuoni hapo na baadaye mbuga za wanyama Mikumi, Dar es Salaam na kuhitimisha huko Zanzibar.

Hii balaa


Kumbe mko 'fit'

Mtaalamu wa masuala ya ukaguzi kutoka nchini Uingereza Dk. Sarah Carthew akikagua chumba cha Habari katika chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM). Hii ni wakati alipofanya ziara ya kukagua maeneo mbalimbali ya chuo hicho.

Monday 31 March 2008

Watoto wa kizungu nao!


Za Mwizi arobaini

Baadhi ya wananchi wenye hasira 'wakimsulubu' mwizi baada ya kumkwapua mwanamama pochi yake. hii ilitokea maeneo ya Msamvu Morogoro.

Wana MUM katika Maulid








Picha zote zinawaonesha wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM) wakiwa katika maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) chuoni hapo.

Duu huyu jamaa tena!


Sunday 30 March 2008

Kipindupindu kitaisha?


Mambo ya Wiki ya Maji

Hii ilikuwa katika Wiki ya Maji viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo usafi umepewa kipaumbele hususan wakati wa kwenda chooni.

Jakaya na wanadiplomasia

Hapa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na wahitimu wa Chuo cha Mahusiano ya Kimataifa na Diplomasia Kurasini Dar es Salaam. Mimi ni wa pili kushoto.

Duuh! mtoto naye


Mambo ya ngoma