Wanafunzi wa Mawasiliano ya Umma mwaka wa tatu, Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro wakifuatilia Mhadhara wa Shaka Ssali Mtangazaji wa VOA (hayupo pichani)
Mtangazaji wa Sauti ya Amerika (VOA) alipotembelea Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro, mwishoni mwa mwaka 2007. Hapa anaongea na vijana wa Mawasiliano ya Umma mwaka wa tatu (hawapo pichani)
Hapa ni Morogoro kwenye maonesho ya Nanenane 2007. Pichani ni kijana wa Muslim University of Morogoro Bashir Salum akijipima nguvu kwa kunyanyua Papai. Haya mambo yanawezekana kama wakulima wetu wakiwezeshwa.
Mbunge wa Same Mashariki (CCM) Mheshimiwa Anne Kilango Malecela akimtwisha mtoto ndoo ya Maji. Anaye 'pampu' maji ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Zanzibar Bi. Castico. Miradi kama hii ni muhimu kwa mustakbali wa wananchi wetu haswa wa vijijini. Hapa ni Kijiji cha Kihurio Same Mkoa wa Kilimanjaro.