Saturday 29 November 2008

Mambo ya Mahafali

Hii ilikuwa ni muda mchache baada ya kutunukiwa shahada ya kwanza ya Mawasiliano ya Umma nikiwa na wenzangu Abdulwakil Saiboko na Simba Shaaban.

Ben Mkapa

Rais mstaafu wa Serikali ya awamu ya tatu Benjamin Mkapa naye hakuwa nyuma katika mahafali ya kwanza ya Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM)

Mambo ya Shampeeeni

Hapa nilikuwa katika hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili yangu baada ya kutunukiwa shahada ya kwanza ya Mawasiliano ya Umma (BA Mass Communication) katika chuo cha Waislamu Morogoro.